Seyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Jumatano alielekea Syria kwa mwaliko rasmi wa rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa maafisa wa kisiasa na kiuchumi.Kutokana na ziara hiyo ya Rais Raisi nchini Syria, Vedant Patel, naibu msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani ametangaza msimamo wa Washington kuhusiana na ziara hiyo, alipozungumza na waandishi wa habari na kueleza kwamba, wanatiwa wasiwasi na kuzidi kuimarika uhusiano kati ya Tehran na Damascus.Katika muendelezo wa madai ya Ikulu ya White House na bila kutaja uvamizi, ukaliaji ardhi kwa mabavu, vita na hatua haribifu za Washington katika eneo la Asia Magharibi na duniani kwa ujumla, Patel amedai kuwa: serikali za Iran na Russia zimeendelea kuchukua hatua haribifu na za kuvuruga utulivu katika eneo hili.
Kufuatia kauli na msimamo huo wa Washington, Nasser Kanani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akiashiria wasiwasi ulioonyeshwa na Marekani kuhusiana na ziara ya Rais Ebrahim Raisi nchini Syria na matokeo yak safari hiyo kwamba: kukasirika utawala muovu uliovunjwa pembe zake na Iran na mhimili wa Muqawama nchini Syria na katika eneo zima, na ambao unapaswa ukomeshe uwepo wake wa kichokozi nchini Syria, ni jambo la kutarajiwa.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza na kuihutubu Marekani: "Kasirikeni na kufeni kwa hasira".../
342/